Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Alikuja katika dunia hii, Akasulubiwa, na Akavumilia dhihaka, dharau, na mateso kutoka kwa watu wasiohesabika. Walakini, Alivumilia haya yote kimyakimya ili kwamba Apate kuwapata watu Wake wa kweli, Afanye upatanisho wa dhambi zao zote, na kuwaokoa.
Katika mchakato wa kuokoa watoto wa mbinguni, Yesu wakati wa ujio Wake wa kwanza, Kristo Ahnsahnghong katika ujio Wake wa pili, na Mama wa Mbinguni Yerusalemu wote Walikuja katika dunia hii katika mwili. Kulingana na unabii, bila shaka njia hii inajumuisha siku za huzuni, zikifuatiwa na siku za shangwe utukufu unapopokelewa. Sambamba na ahadi hii, utukufu wa Mungu Mama, ambaye sasa Analiongoza Kanisa la Mungu, unafunuliwa ulimwenguni kote.
[L]akini Yesu akawaambia, “Nimewaonyesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni ipi katika hiyo mnataka kunipiga mawe?” Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa sababu ya mambo mema uliyotenda, bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ingawa ni mwanadamu unajifanya kuwa Mungu.” Yohana 10:32–33
Jua lako halitazama tena, nao mwezi wako hautafifia tena; BWANA atakuwa nuru yako milele, nazo siku zako za huzuni zitakoma. Isaya 60:20
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA 
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha