Tunapoishi maisha ya kutii sheria ya Mungu, baraka tele sikuzote zimehifadhiwa kwetu. Kwa sababu hii, ndani ya sikukuu ambazo Mungu Alizianzisha tangu enzi ya Baba—kama vile Sabato na Pasaka—sikuzote kuna amri, “Msiyasahau, bali yakumbukeni na kushika milele.”
Biblia inasema kwamba wale wanaoshika sheria ya Mungu katika nyakati zote watabarikiwa kuwa wenye haki, na kwamba wale wanaovunja sheria ya Mungu watahukumiwa kwa sababu ya uasi. Sababu ya Waisraeli kuchukuliwa mateka Babeli ni kutoishika sheria ya Mungu.
“Hatukumtii BWANA Mungu wetu wala kuzishika sheria alizotupa kupitia kwa watumishi wake manabii. Israeli yote imekosea sheria yako na kugeuka mbali, nao wamekataa kukutii. “Kwa hiyo laana na viapo vya hukumu vilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, mtumishi wa Mungu, vimemiminwa juu yetu, kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako.” Danieli 9:10–11
“Huzifuata amri zangu na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu. Huyo mtu ni mwenye haki; hakika ataishi, asema BWANA Mwenyezi.” Ezekieli 18:9
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha